Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya shauku, woga na unyenyekeaji ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.” (al-Anbiyaa´ 21 : 90)

MAELEZO

Yote hayo ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Mitume na waja wema:

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.” (21:90)

Bi maana walikuwa na khofu, wakimuogopa Allaah. Wakimkhofu, bi maana wakimdhalilikia, kwa ukubwa Wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 35
  • Imechapishwa: 20/12/2016