Sayyid Qutwub hana uhusiano wowote na Tawhiyd, wanachuoni wa Tawhiyd wala vitabu vya Tawhiyd. Kwa ajili hii ndio maana utamuona anachanganya maana ya haki ya Allaah kuabudiwa (Uluuhiyyah), uola (Rubuubiyyah), Majina na Sifa na mambo mengine ya khatari katika dini ya Allaah. Hili linatokana na kwamba anajiingiza katika kukifasiri Kitabu cha Allaah bila ya elimu wala ´Aqiydah sahihi. Badala yake amefanya hayo kwa I´tiqaad batili zilizojaa mlima. Harejei kwa wafasiri wa Qur-aan wa Salaf inapokuja katika Tawhiyd na ´Aqiydah. Hazirejelei anapofasiri shahaadah. Kwa ajili hiyo ndio maana tafsiri yake ya Aayah za Tawhiyd inazingatiwa kuwa ni aina moja wapo ya ukengeushaji.

Ni vipi basi anafahamu maana ya “Laa ilaaha illa Allaah”?

Ni vipi basi anafahamu tofauti ya uola wa Allaah na haki ya Allaah ya kuabudiwa?

Ni vipi basi anasalimika na I´tiqaad potevu?

Natumai utaacha kuwa na msimamo wa kupindukia kwa mtu huyu na wengine na utaacha kueneza upetukaji huu kati ya waislamu. Ummah unateseka sana kwa sababu ya fikira za mtu huyu na watu mfano wake. Una haja kubwa ya mtu ambaye atauokoa kutokamana na mabalaa haya.