Swali 23: Ni ipi hukumu ya mwenye kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga? Inajuzu kwa msafiri ikiwa hakufunga kumjamii mke wake?

Jibu: Ni lazima kwa aliyemjamii mke wake mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga atoe kafara. Namaanisha kafara kama ile ya kumfananisha mke na mama pamoja na kulipa siku hiyo, kutubu kwa Allaah (Subhaanah) kutokana na kile kilichomtokea. Ama akiwa msafiri au mgonjwa mwenye maradhi yanayomruhusu yeye kutofunga, basi hakuna juu yake kafara na wala hana dhambi. Lakini hata hivyo atapaswa kuilipa siku hiyo aliyofanya jimaa. Kwa sababu msafiri na mgonjwa inafaa kwa wao wawili kuacha kufunga kwa sababu ya jimaa au sababu nyingine. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Mwanamke katika hili ana hukumu moja kama mwanaume ikiwa swawm yake ni ya lazima. Basi atapaswa kutoa kafara pamoja na kulipa siku hiyo. Akiwa na yeye ni msafiri au mgonjwa mwenye ugonjwa ambao swawm itakuwa ngumu kwake iwapo atafunga, basi juu yao kutakuwa hakuna kafara.

[1] 02:184

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 28
  • Imechapishwa: 06/05/2019