23. Kutumia vidonge vya kuzuia hedhi ili kufunga na wengine


Swali 23: Ni yepi maoni yako juu ya kutumia vidonge vya kuzuia ada ya mwezi kwa ajili ya kufunga pamoja na wengine?

Jibu: Mimi natahadharisha jambo hilo. Hili ni kwa sababu tembe hizi zina madhara makubwa. Hayo yamethibiti kupitia madaktari. Mwanamke anatakiwa kuambiwa kwamba hilo ni jambo ambalo Allaah amewaandikia wasichana wa Aadam. Hivyo basi kinaika na yale ambayo Allaah (´Azza wa Jall) amekuandikia. Funga pale ambapo hakuna kikwazo. Funga wakati hakuna kikwazo. Kukipatikana kikwazo basi kula hali ya kuridhia aliyokadiria Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 20
  • Imechapishwa: 09/07/2021