23. Kumswalia Mtume (صلى الله عليه وسلم) baada ya Tashahhud

53-

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على [إبراهيم و على]آل إبراهيم، إنك حميد مجيد. اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على [إبراهيم و على]آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu [Ibraahiym na] jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki [Ibraahiym na] jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

54-

اللهم صل على محمد و [على]أزواجه و ذريته كما صليت على [آل]إبراهيم، و بارك على محمد و [على]أزواجه و ذريته كما باركت على [آل]إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na wakeze na kizazi chake kama Ulivyowasifu [jamaa za] Ibraahiym. Na mbariki Muhammad na wakeze na kizazi chake kama Ulivyowabariki [jamaa za] Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[2]

[1] al-Bukhaariy pamoja na ”al-Fath” (06/408).

[2] al-Bukhaariy pamoja na ”al-Fath” (06/407) na Muslim (01/306) na tamko ni lake.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 18/02/2020