23. Kuiadhimisha mipaka ya Allaah ni katika ´ibaadah kubwa

Allaah (Ta´ala) amesema:

كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

Hivyo ndivyo Allaah anavyobainisha Aayah Zake kwa watu ili wapate kumcha.”[1]

Bi maana kama ambavyo Allaah amekubainishieni vilevile mipaka ya swawm na ya mambo mengine. Katika baadhi ya Aayah kumebainishwa shari ili iepukwe na Aayah zengine zimebainisha yenye kuruhusiwa ili watu waweze kuyatekeleza. Ni wajibu kwetu kusimama katika mipaka ya Allaah. Yale ambayo Allaah ameturuhusu hakuna ubaya kuyafanya. Yale ambayo ametukataza ni wajibu kwetu kuyaepuka na kuyaogopa. Ni juu yetu kutekeleza faradhi za Allaah kama alivyotaka Allaah na wajibu kwetu kujiepusha na makatazo ya Allaah, ili Allaah awe radhi na sisi na tuwe ni wenye kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 02:187

Mwisho

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 02/06/2017