23. Kinachofanywa siku ya kufuata ya ndoa


21- Kinachotakiwa kufanywa siku ya pili yake

Imependekezwa kwa mume siku ya pili yake akawatembelee jamaa zake [yeye mume] ambao walikuja kumtembelea nyumbani kwake, awasalimie na awaombee du´aa na wao pia imependekezwa kumfanyia vivyo hivyo kutokana na Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitengeneza chakula asubuhi ya usiku wa harusi ambapo akawalisha waislamu mikate na nyama. Kisha akawaendea mama za waumini ambapo akawatolea salamu, akawaombea du´aa ambapo nao wakamuitikia salamu na wakamuombea du´aa. Hivyo ndivyo alivyokuwa akifanya asubuhi ya ndoa yake.”[1]

[1] Ameipokea Ibn Sa´d (08/107), an-Nasaa´iy katika “al-Waliymah” (02/66) kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 19/03/2018