23. Hivi ndivo wanavyoonelea wafuasi wa Juhaymaan suala hili

Kusema kwamba baadhi ya ambao wanajuzisha uasi wameponda mapokezi kama yafuatayo:

“Sikiliza na umtii kiongozi hata kama utapigwa bakora mgongo wako na zikachukuliwa mali zako. Sikiliza na utii!”[1]

Imepokelewa na Abu Sallaam kupitia kwa Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) na inapondwa na wafuasi wa Juhaymaan. Upondaji unatokana na kwamba pindi al-Muzaniy alipotaja ni kina nani Abu Sallaam alipokea kutoka kwao na akamtaja Hudhayfah. Muslim akasema:

“Kuna Swahabah amekosekana katika cheni ya wapokezi.”[2]

 adh-Dhahabiy amesema:

“Amehadithia kutoka kwa Hudhayfah, Thawbaan, ´Aliy, Abu Dharr na ´Amr bin ´Abswah. Mengi katika hayo yaliyopokelewa kuna Swahabah aliyekosekana katika cheni ya wapokezi, kama walivyo wapokezi wa Shaam ambao hupokea kutoka kwa wakubwa.”[3]

Katika taaliki za “Tahdhiyb-ul-Kamaal” imekuja:

“Hakusikia chochote kutoka kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) wala wenzake ambao waliishi ´Iraaq. Kwa sababu Hudhayfah alikufa nyusiku chache baada ya kuuliwa kwa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh).”

Hata kama upokezi huu ni dhaifu makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kufanya uasi dhidi ya watawala yako palepale. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kufanya uasi dhidi ya mtawala na akafa, basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”[4]

Mtu kama huyu atakutana na Allaah akiwa hana hoja yoyote. Ni wajibu kuwapiga vita na kuwaua wenye kufanya uasi midhali mtawala bado ni muislamu, anaswali na hajafanya ukafiri wa wazi kabisa. Hayo yamesihi kutoka kwa ´Ubaadah bin as-Swaamit, Ibn ´Abbaas, Ibn ´Umar, Abu Hurayrah, Abu Sa´iyd, ´Arfajah al-Kilaabiy, Umm Salamah, ´Awf bin Maalik na ´Abdullaah bin ´Amr. Mapokezi yote haya ni Swahiyh yamepokelewa na Muslim katika mlango unaozungumzia uongozi. Kwa hivyo yale yaliyokuja katika ule upokezi dhaifu yamekuja katika mapokezi Swahiyh kutoka kwa Maswahabah tisa. Hakuna anayejuzisha uasi isipokuwa tu mjinga kwa sababu tu upokezi fulani ni dhaifu.

al-Albaaniy amezitaja Hadiyth hizi katika vitabu vyake. Hawezi kusema jengine isipokuwa yale yaliyomo humo. Nina uhakika juu ya hilo kwa sababu tunamtambua namna anavyoshikamana barabara na Sunnah. Hata kama hakukingwa na kukosea; yeye ni kama wanachuoni wengine wote.

[1] Muslim (1847).

[2] Tahdhiyb-ul-Kamaal (28/484).

[3] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (4/355).

[4] al-Bukhaariy (7053) na Muslim (1849).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 44-46
  • Imechapishwa: 03/12/2018