23. Hapa ndipo itakuwa ni sawa kujadili


Imaam Ahmad amesema:

“… na hakuna kitu katika Yeye ambacho kimeumbwa. Ninakutahadharisha na kujadiliana na wale waliozua katika suala hili.”

Tazama namna anavyosisitiza. Lakini pamoja na hivyo yeye mwenyewe alijadili wakati alipohitajia kufanya hivo. Wakati alipolazimika alijadiliana na Ibn Abiy Du´aad na wengine. Ni sawa kujadili wakati wa dharurah, haja na watu wenye kutaka kujifunza na wenye kutaka haki.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 386
  • Imechapishwa: 13/08/2017