23. Dalili ya ishirini na moja kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

21- Muhammad ametukhabarisha: Hamad ametuhadithia: Ahmad ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin as-Sindiy ametuhadithia: Ja´far bin Muhammad bin as-Sabbaah ametuhadithia: Yahyaa bin Khidhaam bin Mansuur ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah bin Ziyaad al-Answaariy ametuhadithia: Maalik bin Diynaar ametuhadithia, kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jibriyl (´alayhis-Salaam) amenikhabarisha kutoka kwa Allaah  (´Azza wa Jall) ya kwamba (Ta´ala) anasema: “Ninaapa kwa nguvu Zangu, utukufu Wangu na umoja Wangu, viumbe Wangu kunihitajia, kulingana Kwangu juu ya ´Arshi na kwa nafasi Yangu kuwa juu ya kwamba Mimi naona haya kumuadhibu mja Wangu wa kiume na wa kike ambao wamepatwa na mvi katika Uislamu.” Hapo ndipo nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akianza kulia ambapo nikamuuliza: “Ni kipi kinachokuliza?” Akajibu: “Nalia juu ya yule ambaye Allaah (Ta´ala) anamuonea haya lakini yeye hamuonei haya Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] Hilyat-ul-Awliyaa’ (2/387). adh-Dhahabiy amesema:

”Inaingia katika idadi ya Hadiyth zilizozuliwa. al-Answaariy huyu sio mwaminifu.” (al-´Uluww, uk. 43)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 103
  • Imechapishwa: 03/06/2018