23. Dalili juu ya mkono wa Allaah 9


23- Ismaa´iyl bin Muhammad bin Ismaa´iyl an-Nahawiy ametuhadithia: Ahmad bin Mulaa´iyb ametuhadithia: ´Umar bin Hafsw bin Ghayyaath ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia: Nimemsikia Ibraahiym akisema: Nimemsikia ´Alqamah akisema: ´Abdullaah amesema:

“Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Hakika Allaah (´Azza wa Jall) atazizuia mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, milima kwenye kidole, miti na ardhi kwenye kidole na viumbe kwenye kidole. Kisha Aseme: “Mimi ndiye Mfalme! Mimi ndiye Mfalme!” Nikamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyocheka mpaka magego yake yakaonekana. Halafu akasoma:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Umar bin Hafsw bin Ghayyaath kutoka kwa baba yake.

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 27/02/2018