116- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utajiri sio wa kuwa na pesa nyingi. Utajiri ni wa moyo.”[1]

117- Inasemekana kuwa dunia utupu uliopo wenye kuliwa na mtu mwema na mtenda dhambi. Allaah (Ta´ala) amesema:

تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا

“Mnataka vitu vya dunia.” (08:67)

Bi maana utajiri wenye kunufaisha, mkubwa au utajiri wenye kusifika unapatikana kwenye nafsi ya tajiri.

118- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye hamu yake kubwa ni dunia basi Allaah humfanyia jambo lake kufarikana na huweka ufakiri kwenye macho yake na hatopata katika dunia isipokuwa kile Allaah alichomwandikia. Na yule ambaye hamu yake ni Aakhirah basi Allaah humkusanyia jambo lake na huweka utajiri kwenye moyo wake na dunia hii itamjia kwa nguvu.”[2]

119- Wanachuoni wanasema mazungumzisho katika mlango ni kwamba mtu haimfai akawa ni mwenye tamaa na mroho. Kitu chenye kutoa dalili ya kuonyesha moyo tajiri ni kukinaika na kuridhika na kile mtu alichonacho na kuwa na wasiwasi juu ya yale yenye kumsubiri huko Kwake mwenye kuumba sababu na sio sababu yenyewe.

[1] al-Bukhaariy (6446) na Muslim (1051).

[2] Ibn Maajah (4105), Ahmad (5/183) na Ibn Hibbaan (72). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (2/671).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 77-79
  • Imechapishwa: 18/03/2017