Swali 22: Je, tusikemee na kuwabainishia watu kosa lilioko ndani ya gazeti?

Jibu: Kosa lilioko ndani ya gazeti au hata kwa watu halitatuliwi misikitini wala juu ya minbari. Lakini hata hivyo ni sawa kulikemea kosa kwa njia ya ujumla pasi na kumlenga mtu. Hivyo ndivyo alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo kama hicho kina manufaa bila ya madhara. Ikiwa kuna kosa ndani ya gazeti au kwa mwandishi, raddi gazeti au mwandishi na utume Radd hiyo kwenye gazeti. Ikiwa gazeti hilo haikueneza Radd hiyo itume kwenye gazeti nyingine. Kwa njia hiyo kunapatikana ufumbuzi[1].

Ama kukusanya magazeti na kuyaleta msikitini au kwenye Khutbah ya ijumaa na kuyasoma juu ya minbari, hiyo maana yake ni kwamba unawafunza watu shari, kueneza moavu na kuwafedhehesha wale watenda madhambi.

[1] Huu ndio mfumo wa Salaf ambao inatakikana kwa mlinganizi kuutendea kazi pindi anapokemea kosa; kwa kuraddi na kuandika. Hata hivyo haitakikani kuyanyamazia makosa, ni jambo la wajibu kuihami Shari´ah – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy