22. Sababu ya ishirini na moja ya maisha mazuri: Kiyapa kipaumbele yale mambo yenye umuhimu zaidi

21- Unatakiwa kuchagua katika yale mambo yenye manufaa jambo lenye umuhimu mkubwa zaidi kisha linalofuata katika umuhimu na pambanua katika mambo hayo lile ambalo nafsi yako imeegemea zaidi na shauku yako inakuwa kubwa zaidi. Kwani kinyume chake kitakufanya kuchoka na kuchafuka kwa nafsi. Wakati wa kufanya hivo taka msaada kwa fikira ambazo ni sahihi na ushauri. Kamwe hajutii yule aliyetaka ushauri. Yasome yale unayotaka kuyafanya masomo ya ndani kabisa. Pindi yatapohakikika manufaa na ukaazimia basi mtegemee Allaah, kwani hakika Allaah anawapenda wale wenye kumtegemea.

Himdi zote ni stahiki za Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salamu zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 32
  • Imechapishwa: 06/07/2020