89- Ili uweze kukanusha uwezekano kunahitajia kuwepo kwa dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah. Kwani sifa za Allaah hazithibitishwi wala kupingwa isipokuwa kwa dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah. Ikishakuwa hakuna uwezekano huo basi inabatilika kuthibitisha ueneaji kwa njia ya usahihi ambao unapaswa kuaminiwa kwa mujibu wa ulengeshaji wa yule mzugumzaji. Imepokelewa kwamba Imaam Muhammad bin Idriys ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Naamini yale yaliyokuja kutoka kwa Allaah kama alivokusudia Allaah na naamini yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume wa Allaah kama alivokusudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

90- Hii ndio njia ilionyooka na ´Aqiydah sahihi na iliosalimika isiyomweka mwenye nayo kwenye khatari wala aibu. Kwani hakuna jengine alichofanya isipokuwa kuamini yale yaliyomo ndani ya Qur-aan na Sunnah, jambo ambalo ndilo la wajibu kwa viumbe wote. Kwani akikanusha neno hata moja ndani ya Qur-aan ambalo kuna maafikiano juu yake basi anakufuru kwa maafikiano ya waislamu. Kuacha kulifasiri pasi na dalili sahihi juu ya tafsiri hiyo ni jambo la wajibu kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maafikiano. Na kama isingekuwa ni jambo la wajibu basi angalau kwa uchache ingekuwa ni jambo linalojuzu. Hilo ni jambo lisilokuwa na tofauti yoyote.

91- Isitoshe jengine ni kwamba hiyo ina maana ya kufuata Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwafuata wale waliobobea katika elimu na Salaf katika Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na maimamu. Kwa njia hiyo mtu anakuwa amesalimika kuzungumza juu ya Allaah, Kitabu Chake na sifa Zake yale asiyoyajua au kutokana na mtazamo wake mwenyewe. Pia isitoshe mtu anakuwa ameepuka kumsifu Allaah kinyume na vile alivyojisifu Mwenyewe au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ambavo anakuwa amesalimika kukanusha sifa ambayo amejithibitishia nayo Mwenyewe na Mtume Wake.

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 11/01/2021