22. Mtume alifikwa na yepi kutoka kwa washirikina?

Swali 22: Alifikwa na yepi yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na watu wa nyumbani kwake kutoka kwa washirikina wa ki-Quraysh?

Jibu: Washirikina hawakuacha kumuudhi mpaka mwishowe wakaafikiana kumuua. Allaah akamlinda kwa ami yake Abu Twaalib ambaye akaikusanya familia yake na ukoo wake Banuu Haashim na Banuu ´Abdil-Muttwalib. Makafiri na waumini wao wote wakaafikiana kumtetea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtanguliza yeye mbele ya nafsi zao. Mtu pekee aliyepinga alikuwa Abu Lahab – iangamie mikono yake miwili!

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 18/09/2023