Mwanamke mwema hujitahidi kushinda mapenzi ya mume wake kwa kumpambia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu wanawake bora ambapo akajibu:

“Ni yule anayemtii mume wake pindi anapomuamrisha na kumfurahisha pindi anapomtazama.”[1]

Hasemi kitu asichopenda mume wake kusikia. Haonyeshi kitu kinachomuudhi mume kuona. Hayo hayapitiki hata kwa maneno. Mwanamke mwema alobarikiwa anaogopa kumuudhi mume wake kwa neno hata moja, mtazamo, ombi, kitendo kimoja au muonekano mbaya. Kwa nini? Kwa sababu anajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mwanamke anayemuudhi mume wake duniani isipokuwa husema mke wake katika al-Huur al-´Ayn: “Usimuudhi, Allaah Akuue! Hakika huyo kwako ni mgeni tu. Anakaribia kukuacha ili awe na sisi.”[2]

[1] an-Nasaaiy (3231), Ahmad (2/251) na al-Haakim (2/2682) ambaye ameisahihisha kwa mujibu wa masharti ya Muslim. Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (1838) na ”al-Irwaa’” (1786).

[2] at-Tirmidhiy (1174), Ibn Maajah (2014) na Ahmad (5/242). Nzuri na geni kwa mujibu wa at-Tirmidhiy. Mnyororo Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (173).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 35
  • Imechapishwa: 24/03/2017