5- Majina yanayoafikiana na ule utoaji wa majina kwa mujibu wa masharti na adabu za majina.

Sunnah inabainisha kuwa jina kwa mujibu wa Shari´ah linatakiwa kutimiza masharti mawili:

1- Jina linatakiwa kuwa la kiarabu. Hapa kunatoka majina yote yaliyotolewa nje.

2- Linatakiwa kutamkwa vizuri na liwe na maana nzuri. Hapa kunatoka majina yote ya haramu na yaliyochukizwa pasi na kujali kama uharamu au machukizo hayo yanatokamana na matamko yake, maana yake au vyote viwili. Vivyo hivyo ikiwa jina ni la kiarabu lakini lina kujitakasa, lawama au matusi.

at-Twabariy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Haifai kutoa jina lililo na maana mbaya, ya kujitakasa wala lililo na maana ya kutukana ingawa inahusiana tu na jina lisiloafikiana kabisa na sifa za mtu huyo. Machukizo yanakuja kwa njia ya kwamba mtu anasikia jina hilo na anadhania kwamba yule mpewaji ana sifa zake. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha jina kwa kile chenye kuafikiana na yule mzungumzishwaji.”

at-Twabariy amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha majina mengi.”[1]

[1] Fath-ul-Bariy (10/476).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 18/03/2017