22. Maneno ya Allaah hayakutengana Naye

Imaam Ahmad amesema:

“Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Mtu asidhoofike kusema kuwa hayakuumbwa. Hakika maneno ya Allaah hayakutengana Naye na hakuna kitu katika Yeye ambacho kimeumbwa.”

Maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ni sifa iliyosimama katika dhati Yake, lakini anazumgumza pale anapotaka na akitaka. Maneno ya Imaam Ahmad:

“Hakika maneno ya Allaah hayakutengana Naye… “

anawaraddi Mu´tazilah wenye kusema kuwa Allaah aliyaumba bila ya sehemu. Maneno ya Allaah ni sifa kama mfano wa uwezo na utashi Wake ambavyo ni sifa za milele zilizosimama kwenye dhati Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni sifa kamilifu. Allaah anazungumza pale anapotaka kama jinsi Anavyoumba wakati anapotaka:

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

“Hakika amri Yake anapotaka kitu hukiambia: “Kuwa!” –  na kikawa.”[1]

Maneno ni sifa ya dhati, lakini anazungumza, anafunua, anaumba na anaruzuku kwa maneno Yake. Maneno ya Imaam Ahmad:

“Hakika maneno ya Allaah hayakutengana Naye… “

anachokusidia ni kwamba maneno Yake yamesimama kwenye dhati Yake. Pamoja na hivyo Qur-aan na maneno Yake yanasikika. Yaani maneno ya Ahmad:

“Hakika maneno ya Allaah hayakutengana Naye… “

analenga kwamba ni sifa iliyosimama katika dhati Yake, akiwaraddi Mu´tazilah wenye kusema kuwa Allaah ameumba maneno bila ya sehemu.

[1] 36:82

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 385-386
  • Imechapishwa: 13/08/2017