22. Kikosi cha kijeshi cha al-´Ushayrah


Baada ya hapo kulikuwa na kikosi cha al-´Ushayrah, ambapo pia kinaitwa al-Usayrah na ”al-´Ushayraa””. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia alishiriki katika Jumaadaa al-´Uulaa. Sehemu hiyo ipo katika bonde la Yanbu´. Alibaki huko mwezi ulobaki na siku mbili katika Jumaadaa al-Aakhirah. Akafanya mkataba wa amani na Banuu Majd kisha akarudi na hakukutokea vitimbi. al-Madiynah alikuwa amemuacha Abu Salamah bin ´Abdil-Asad (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa khalifa. Muslim amepokea katika ”as-Swahiyh” yake kwamba Abu Ishaaq as-Sabi´iy amesema:

”Nilisema kumwambia Zayd bin Arqam: ”Ni misafara ngapi ya kijeshi alishiriki Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: ”Ni misafara tisa. Wa kwanza ulikuwa al-´Ushayrah, au al-´Ushayraa´.”

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 43
  • Imechapishwa: 26/04/2018