22. Iogopeni mipaka ya Allaah


Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ

“Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi ni wenye kukaa I’tikaaf  misikitini.”[1]

Haya ni makatazo kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Mtu anayefanya I´tikaaf haijuzu kwake kufanya jimaa na wanawake na wala haijuzu hata kubusu. Mzee aliye na matamanio dhaifu inafaa kwake kubusu. Lakini mtu anayefanya I´tikaaf haifai kwake kubusu wala kukumbatia katika hali yoyote. Hayo ni haramu. Allaah (Ta´ala) amesema:

تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ

“Hiyo ni mipaka ya Allaah.”[2]

Kitendo hichi ni katika mipaka ya Allaah. Yule mwenye kuchanganyika na mwanamke iliali ni mwenye kufanya I´tikaaf amevuka mpaka wa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا

“Hiyo ni mipaka ya Allaah, hivyo basi msiikaribie.”[3]

Hii ni dalili inayofahamisha kuwa ni haramu kuchanganyika na wanawake wakati wa I´tikaaf na ni moja katika mipaka ya Allaah aliyoiharamisha.

[1] 02:187

[2] 02:187

[3] 02:187

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 02/06/2017