Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Mwisho wake: Himdi zote ni Zake Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake mpaka siku ya Qiyaamah.

MAELEZO

Amemalizia kitabu hiki kama jinsi alivyouanza kwa kumhimidi Allaah na kumswalia Mtume Wake. Huu ni katika uzuri wa kutunga na kufunza kwa kule mtu kumsifu Allaah mwanzoni na mwishoni.

Swalah na amani zimwendee Mtume Wake, mwalimu wa mambo ya kheri na mlinganizi katika dini ya Allaah. Ee Allaah msifu katika ulimwengu wa juu, waswalie familia yake, Maswahabah zake na yule mwenye kufuata uongofu wake na akapita katika mfumo wake na akashikamana na Sunnah zake mpaka siku ya Qiyaamah. Himdi zote ni Zake Yeye Allaah, Mola wa walimwengu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 44
  • Imechapishwa: 19/05/2021