22. Du´aa wakati muumini anaposibiwa na kitu kidogo au kikubwa

Allaah (Ta´ala) Amesema:

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ

Wale ambao unapowafika msiba husema: “Innaa liLLaahi wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn” (Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea). Hao juu yao zitakuwa Baraka kutoka kwa Mola wao na Rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.” (al-Baqarah 03 : 156-157)

114- Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ´anha) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

إِنَّا لله وإِنَّا إِلَيْه راجعونَ اللهُمَّ أَجِرْني في مُصِيبَتي وَأَخْلِفْ لي خَيْراً منها

“Sisi ni wa Allaah na Kwake ndipo tutarejea. Ee Allaah! Nilipe kwa ujira wangu na nipe bora kuliko hichi.”

isipokuwa humlipa kwa msiba wake na kumpa bora kuliko kitu hicho.”

Ummu Salamah amesema:

“Wakati Abu Salamah alipofariki nikasema kama alivyoniamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Allaah Akanipa aliyebora kuliko yeye; Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

115- Ummu Salamah amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa Abu Salamah. Macho yake yalikuwa yamefumbwa, akayafunga na kusema: “Roho inapochukuliwa macho hufuata.” Watu katika familia yake wakapandisha sauti. Hivyo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Msijiombee dhidi yenu na msiombe isipokuwa kheri tu. Hakika ya Malaika huitikia “Aamiyn” kwa yale mnayoyasema.” Halafu akasema: “Ee Allaah! Msamehe Abu Salamah na inyanyue daraja yake kwa walioongoka na kipe kizazi chake kilichobaki kiongozi. Tusamehe sisi na yeye, ee Mola wa walinwengu! Mpanulie kaburi lake na mtilie nuru.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 21/03/2017