22. Damu inayomtoka mjamzito kabla ya kuzaa


Swali 22: Mjamzito akiona damu kabla ya kuzaa kwa siku moja au mbili – je, aache kufunga na kuswali kwa ajili yake au afanye nini?

Jibu: Mjamzito akiona damu kabla ya kuzaaa kwa siku moja au mbili na damu hiyo ikaambatana na kuhisi uchungu, basi hiyo ni damu ya uzazi. Basi kwa ajili yake aache kuswali na kufunga. Ikiwa haitoambatana na uchungu basi hiyo ni damu fasidi. Haizingatiwa na wala haitomzuia kutokamana na kufunga na kuswali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 08/07/2021