22. Dalili za kujifunika ni zenye kutangulizwa juu ya dalili za kujifunua

Lakini hata hivyo dalili hizi hazigongani na dalili zenye kuwajibisha Hijaab kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na:

Mosi: Dalili za kujifunika ni zenye kutoka kwenye kianzio wakati dalili zenye kujuzisha kujifunua ziko katika kianzio. Zenye kutoka kwenye kianzio zinapewa kipaumbele juu ya ambazo ziko katika kianzio. Hilo ni kwa sababu kilichoko katika kianzio kinahusiana na kitu kubaki kama jinsi kilivyokuwa. Kunapokuja dalili juu ya kitu chenye kutanua zaidi kutoka kwenye kianzio, basi hiyo ina maana kuwa hukumu ya kianzio imebadilika. Ndio maana tunasema kile chenye kutanua zaidi kutoka kwenye kianzio ni elimu zaidi yenye kuthibitisha ya kuwa ile hukumu asili imebadilika – yenye kuthibitisha ni yenye kupewa kipaumbele juu yenye kupinga.

Mtazamo huu ni wa jumla na imara hata kama itahusiana na dalili zilizo na nguvu sawa kutokana na kuthibiti kwake na ushahidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 30
  • Imechapishwa: 26/03/2017