4- Kufa shahidi katika uwanja wa mapambano. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ  فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ

“Usifikirie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu. Bali wahai kwa Mola wao wanaruzukiwa. Wanafurahia kwa aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanafurahi [kwa bishara wale] ambao [bado] hawajaungana nao walio nyuma yao kwamba hakutokuwa na khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Wanashangilia kwa neema kutoka kwa Allaah na fadhila na kwamba Allaah hapotezi ujira wa waumini.”[1]

Kuhusiana na hilo kumepokelewa Hadiyth zifuatazo:

A- “Shahidi mbele ya Allaah ana mambo sita; husamehewa katika ule mchupo wa kwanza tu wa damu yake, anaona makazi yake kutoka Peponi, analindwa kutokamana na adhabu ya kaburi, atakingwa na mfazaiko mkubwa, atapambwa kwa pambo la imani, ataozeshwa wanawake wa Peponi na atapewa uombezi awaombee watu sabini katika jamaa zake wa karibu.”

Ameipokea at-Tirmidhiy (03/17) na ameisahihisha, Ibn Maajah (02/184), Ahmad (131) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.  Kisha akaitaja (04/200) pia kupitia kwa ´Ubaadah bin as-Swaamitw kupitia kwa Qays al-Judhaamiy (04/200) na cheni za wapokezi wake wawili hao ni Swahiyh.

B- Kutoka kwa Jaabir ambaye amesimulia kutoka kwa mmoja kaitka Maswahabah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesimulia:

“Kuna mtu mmoja alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Vipi waumini watapewa mtihani ndani ya makaburi yao isipokuwa shahidi?” Akamjibu: “Ule ng´ao wa upanga juu ya kichwa chake unatosha kuwa ni mtihani.”

Ameipokea an-Nasaa´iy (01/289) al-Qaasim as-Sarqastwiy katika “Ghariyb-ul-Hadiyth” (02/165/01) kwa cheni ya wapokezi nzuri.

Tanbihi

Kuwa shahidi namna hii kunatarajiwa kwa yule mwenye kumuomba Allaah hali ya kuwa ni mkweli kutoka moyoni mwake. Haijalishi kitu hata kama hakujaaliwa kufa shahidi katika uwanja wa vita. Dalili ya hilo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kumuomba Allaah kufa shahidi kwa ukweli basi Allaah atamfikisha  ngazi za waliokufa mashahidi ijapokuwa atakufa juu ya kitanda chake.”

Ameipokea Muslim (02/49), al-Bayhaqiy (09/169) kutoka kwa Abu Hurayrah.

Ina katika “al-Mustadrak” (02/77) zengine zenye kuitoa ushahidi.

[1] 03:169-171

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 30/01/2020