22. Ahl-ul-Bid´ah waovu zaidi


Kwa mfano unaposoma:

إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[1]

tunasema kuwa Aayah inamthibitishia Allaah sifa ya elimu, ambayo ni sifa ya kidhati, kwa uwazi kabisa na kwa njia inayolingana na ukubwa na utukufu Wake, pasi na kushabibisha, kufananisha, kupindisha maana, kupotosha wala kukanusha. Bali inatakiwa kufahamika kutokana na maneno tukufu ya Mola:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[2]

Sema mfano wa hayo kuhusu sifa zengine zote. Kinachosemwa ni kimoja juu ya sifa zote tukufu za Allaah (´Azza wa Jall).

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema kuwa Mufawwidhwah ndio Ahl-ul-Bid´ah waovu zaidi. Kwa sababu wamesema maneno ya ujinga juu ya Allaah pasi na elimu, wamejizuia kusema haki kuhusu maana ya sifa na wakazipa mgongo – hilo limewafanya pia kuwa wajinga.

[1] 29:62

[2] 42:11

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 75
  • Imechapishwa: 10/10/2019