112- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Moyo wa mzee hupata utulivu kwa kupenda mambo mawili; maisha marefu na mali nyingi.”[1]

113- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Lau mwanaadanu angelikuwa na tende mbili za mali basi angelitamani kuwa na ya tatu. Hakuna kitachojaza tumbo la mwanaadamu isipokuwa udongo na Allaah anamsamehe yule mwenye kutubia.”[2]

114- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbwa mwitu wawili walio na njaa wenye kutumilizwa kwenye kundi la kondoo hawana khatari kwao kuliko pupa ya mtu kwa mali na heshima iko kwa ajili ya dini yake.”[3]

115- al-Madaainiy amesema:

“Sifa mbili hazikutani kamwe; ukinaikaji na hasadi. Sifa mbili hazifarikiani kamwe; pupa na tamaa.”

[1] al-Bukhaariy (11/239) na Muslim (2/724).

[2] Muslim (02/725).

[3] Ahmad (03/456).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 75-77
  • Imechapishwa: 18/03/2017