Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kubwa Alilokataza Allaah ni shirki, nako ni kuomba wengine pamoja Naye. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (an-Nisaa´ 04 : 36)

MAELEZO

Kubwa alilokataza Allaah ni shirki na hilo ni kwa sababu haki iliokubwa ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall). Yule mwenye kufanya upungufu katika suala hili, basi amefanya upungufu katika haki iliokubwa, nayo ni kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall) pekee. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

“Hakika shirki ni dhulma kubwamno!” (Luqmaan 31 : 13)

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemshirikisha Allaah, basi kwa hakika amebuni dhambi kuu.” (an-Nisaa´ 04 : 48)

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Na yeyote atakayemshirikisha Allaah, basi hakika amepotoka upotofu wa mbali.” (an-Nisaa´ 04 : 116)

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemshirikisha Allaah, basi kwa hakika amebuni dhambi kuu.” (al-Maaidah 05 : 72)

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakaye.“ (an-Nisaa´ 04 : 48)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dhambi kubwa ni kumfanyia Allaah mshirika ilihali Yeye ndiye amekuumba.”[1]

Amesema (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) katika Hadiyth ambayo Muslim ameipokea kupitia kwa Jubayr (Radhiya Allaahu ´anh):

“Yule atayekutana na Allaah pasi na kumshirikisha Yeye na chochote, ataingia Peponi, na yule atayekutana na Allaah ilihali ni mwenye kumshirikisha na chochote, ataingia Motoni.”[2]

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kufa ilihali anaomba mshirika badala ya Allaah, basi ataingia Motoni.”[3]

Ameipokea al-Bukhaariy.

Mtunzi wa kitabu ametolea dalili kwamba Allaah (Ta´ala) ameamrisha Tawhiyd na kukataza shirki kwa maneno Yake (´Azza wa Jall):

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.”

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akaamrisha kumwabudu Yeye na akakataza kumshirikisha. Hili linapelekea kuthibitisha ya kuwa ´ibaadah anafanyiwa Yeye pekee. Yule asiyemwabudu Allaah ni kafiri na ni mwenye kiburi, yule mwenye kumwabudu Allaah pamoja na wengine ni kafiri mshirikina na yule mwenye kumwabudu Allaah peke Yake ndiye muislamu mwenye kumtakasia nia.

Kuna aina mbili za shirki:

Shirki kubwa.

Shirki ndogo.

1- Shirki kubwa. Hii ni kila kitu ambacho Shari´ah imeita kuwa ni ´shirki` kwa njia ya kuachia na ikawa inamtoa mtu katika dini.

2- Shirki ndogo. Hii ni kila neno na kila kitendo ambacho Shari´ah imeeleza kuwa ni shirki pasi na kumtoa mwenye nayo katika dini.

Kwa hiyo ni lazima kwa mtu kutahadhari na aina zote za shirki, ni mamoja ikiwa ni kubwa au ndogo. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa.”

[1] al-Bukhaariy (7520), Muslim (141), Abu Daawuud (2308), at-Tirmidhiy (3396), an-Nasaa´iy (4024), Ahmad (1/380) na Ibn Hibbaan (4397).

[2] Muslim (152), Ibn Maajah (2618) na Ahmad (2/362).

[3] al-Bukhaariy (4497) na Ahmad (1/402).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 41
  • Imechapishwa: 20/05/2020