21. Samaki mkunje akingali mbichi

Watoto wanapofunzwa tangu wakingali wadogo basi elimu yao inakuwa yenye kubarikiwa. Elimu ni yenye kuwaathiri zaidi kuliko wanapokuwa wameshakuwa wakubwa. Kwa sababu wamekulia juu ya elimu na inakuwa imekita kwenye mioyo na ubongo wao. Ndio maana utawapata watoto ambao wameleleka juu ya kuhifadhi swalah na mafunzo juu ya ´Aqiydah na dini yao ndio vijana bora kabisa wanapokuwa wakubwa. Lakini wakiachwa na kupuuzwa, basi inakuwa vigumu kwa wazazi wao kuwalea. Mshairi amesema:

Matawi yanaporekebishwa hunyooka

lakini hayawi mepesi ikiwa yameshakuwa mbao

Malezi kwa mtoto bado akingali mdogo unaweza kumrekebisha. Lakini huwezi kumrekebisha akishakuwa mkubwa.

Baada ya hapo akamwambia mwalimu wake:

“Nikakuitikia maombi yako, kwa sababu nataraji mimi na wewe kupata thawabu za kuifunza dini ya Allaah au kulingania kwayo.”

Yule mwenye kulingania katika jambo la kheri ni kama mwenye kulifanya. Yeye na mwalimu wake wote wawili ni wenye kushirikiana katika thawabu, kwa sababu yeye ndiye ambaye kamfunza na kumwelekeza katika jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 23
  • Imechapishwa: 12/07/2021