21. Ni zepi nasaha zako kwa wanafunzi?


Swali 21: Ni zepi nasaha zako kwa mwanafunzi anayeanza na ni vipi vitabu na mikanda unayopendekeza?

Jibu: Wasia wangu kwa wanafunzi wote wamche Allaah (´Azza wa Jall) na wafuate mfumo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Nao si mfumo mwengine ni wa Salafiyyah. Ninawausia kukaa chini kwa wanachuoni Salafiyyuun na wasome vitabu vya Tawhiyd. ´Aqiydah, Hadiyth na vya Fiqh. Mambo yanatakiwa kuwa namna hii.

Ni wajibu kwa wanafunzi wamche Allaah (´Azza wa Jall) na watahadhari na Da´wah hizi za ki-Hizbiyyah. Malengo yazo ni kufarikisha umoja wao na kuwatawanyisha. Hatimaye umoja wao ufarikiane.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametutahadharisha na walinganizi wanaolingania kuelekea Motoni. Ni jambo lisilo na shaka kuwa Hizbiyyah ina makosa mabaya. Hivyo ni wajibu kwa mwanafunzi atahadhari nayo na alazimiane na halaka za wanachuoni Salafiyyuun. Anatakiwa asome vitabu vilivyoandikwa na Salafiyyuun na wakati huo huo atahadhari na vitabu vya Hizbiyyuun. Kwani ndani yavyo mna asali na sumu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017