21. Ni lazima mwanamke kulipa swalah ya ule wakati ametwahirika ndani yake?

Swali 21: Mwanamke akipata hedhi kwa mfano saa saba mida ya adhuhuri na yeye bado hajaswali Dhuhr analazimika kulipa swalah hiyo ya Dhuhr?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya hili. Miongoni mwao wako waliosema kuwa haimlazimu kulipa swalah hii. Kwa sababu hakuzembea na wala hapati dhambi kwa kuwa inafaa kwake kuchelewesha swalah mpaka wakati wake wa mwisho. Wako wanachuoni wengine waliosema kuwa inamlazimu kulipa swalah hiyo kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

dhimmah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah basi ameiwahi swalah.”

Lililo salama zaidi kwake ni yeye kuilipa kwa sababu ni swalah moja peke yake isiyokuwa na uzito katika kuilipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 19
  • Imechapishwa: 06/07/2021