21. Ni kwanini haitoshelezi kusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah?

Imaam Ahmad amesema:

“… na hayakuumbwa.”

Ni kwa nini haitoshelezi kusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah? Kwa sababu Jahmiyyah na Mu´tazilah ambao wanakanusha kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah wanasema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na wakati huohuo wanakusudia kuwa imeumbwa. Kama jinsi wanavyosema “ngamia wa Allaah” na “nyumba ya Allaah”. Nyumba ya Allaah imeumbwa na hali kadhalika ngamia wa Allaah. Wanatumia mfumo huu. Wanawapaka watu mchanga wa machoni wanaposema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah; lakini imeumbwa. Ndio maana watakiwa kusema Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Kwa sababu ukisema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah bila ya kusema kuwa hayakuumbwa, Mu´tazilah na Jahmiyyah wanakubaliana na wewe na wao pia waseme kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah. Hata hivyo wanakamilisha maana yao kwa kusema kuwa imeumbwa wakati wewe unakamilisha maana yako kwa kusema kuwa haikuumbwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 385
  • Imechapishwa: 07/08/2017