21. Ni ipi Njia iliyonyooka na ni zepi sifa zake?

Swali 21: Ni ipi Njia iliyonyooka na ni zepi sifa zake?

Jibu: Njia iliyonyooka ni elimu yenye manufaa na matendo mema.

Elimu yenye manufaa ni yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya Qur-aan na Sunnah.

Matendo mema ni kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) kwa kuwa na I´tiqaad ambazo ni sahihi, kutekeleza mambo ya faradhi na yaliyopendekezwa na kujiepusha na yaliyokatazwa. Kwa msemo mwingine inahusiana na kutekeleza haki za Allaah na haki za waja Wake.

Hakuna chenye kutimia katika hayo isipokuwa kwa kumtakasia nia Allaah na kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dini imejengwa juu ya misingi hii miwili. Asiyeitakasa nia yake anatumbukia katika shirki na asiyemfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatumbukia katika Bid´ah.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com