1- Ikiwa utani unahusiana na madhambi basi hufanya uso kuwa mweusi na moyo kutokwa na damu. Unaeneza chuki na unahuisha uadui. Ikiwa hauhusiani na madhambi unamliwaza yule mwenye hamu, unajenga urafiki, unazihuisha nyoyo na unaondosha heshima. Ni wajibu kwa aliye na busara kutumia mzaha vizuri pasi na kumuudhi yeyote wala kumfurahisha mtu kwa kumuudhi mwengine.

2- Ibraahiym amesema:

“Hakuna anayefanya utani nawe isipokuwa yule anayekupenda.”

3- Muhammad bin al-Munkadir amesema:

“Mama yangu alinambia pindi nilipokuwa mdogo: “Usifanye mzaha na watoto usije ukashuka machoni mwao wakakuparamia.”

4- ´Umar bin al-Khattwaab amesema:

“Mwenye kukithirisha kucheka hupoteza heshima yake Mwenye kufanya mzaha hatochukuliwa kikweli. Mwenye kukithirisha kwa kitu basi hutambulika kwacho.”

5- Mwenye kufanya utani na mtu asiyekuwa katika ngazi yake hushuka machoni mwake na atamparamia hata kama mzaha huo ni haki. Inafaa tu kufanya mzaha na watu wa jinsia ambao mtu anaendana nao.

6-  Mimi nachukia mtu kufanya utani mbele ya ambaye si msomi. Kadhalika nachukia mtu kuacha kufanya utani pindi yuko na watu mfano wake.

7- Abu ´Abdir-Rahmaan al-A´raj amesema:

“Ibraahiym bin Adham alikuwa akituelezea Hadiyth na akitania na sisi. Pale tu anapomuona mtu ambaye si katika sisi, anasema: “Huyu ni jasusi.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 79-81
  • Imechapishwa: 06/02/2018