Kuhusu shirki ni kufanya kitu katika aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Tumetangulia kusema kwamba ´ibaadah ni aina nyingi zinazochukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo basi, yule mwenye kufanya kitu katika aina ya ´ibaadah hizi, basi huyo ni mshirikina ambaye kafanya shirki kubwa inayomtoa katika Uislamu. Mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, akaweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, akasujudu kwa asiyekuwa Allaah, akamuomba asiyekuwa Allaah katika wafu na viumbe vilivyoko mbali, akawataka uokozi wafu n.k., huyu kamshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu ´ibaadah kwa aina zake zote ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Ta´ala):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.”(adh-Dhaariyaat 51:56)

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

”Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (an-Nisaa´ 04:36)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 41
  • Imechapishwa: 04/07/2018