21. Kinafanywa nini kiungo cha mwili kilichokatwa kutoka kwa mtu?

Swali 21: Ni ipi hukumu ya kumkata mtu kiungo maalum kilichozidi kama mfano wa kidole au kiungo kingine? Je, kiungo hichi kikatwe pamoja na taka au kikusanywe na alazimishwe mtu aende kukizika kwenye makaburi ya waislamu?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Kiungo hicho hakina hukumu ya mtu na hakuna makatazo ya kukiweka kwenye taka au kukifukia chini ya ardhi kwa ajili ya kukiheshimu, ambalo ndio bora zaidi. Vinginevyo jambo ni lenye wasaa kama tulivyotangulia kusema. Si lazima kukiosha wala kukizika. Isipokuwa ikiwa ni kipomoko kilichokamilisha miezi mine. Ama kipande cha nyama ambacho hakikupuliziwa roho, kipande cha kidole au mfano wake jambo ni lenye wasaa. Lakini mtu kukizika ndani ya ardhi ilio safi inakuwa ni vyema na bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 44
  • Imechapishwa: 17/08/2019