Allaah (Ta´ala) Amesema kuhusu kisa cha watu wawili:

وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ

“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Maa Shaa Allaah! Laa quwwata illa bilLLaah’ (Ametaka Allaah; hapana nguvu ila za Allaah).” (Aal ´Imraan 03 : 39)

113- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapoona kitu anachokipenda husema:

الحمد لله الذي تَتِمُّ بِنِعْمَتِهِ الصَّالِحَاتُ

“Himdi zote ni Zake Allaah ambaye kwa neema Zake hutimia vizuri.”

Wakati anapoona kitu anachokichukia husema:

الْحَمْدُ للهِ عَلى كُلِّ حال

“Himdi zote ni Zake Allaah kwa kila hali.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 21/03/2017