21. Dalili juu ya mkono wa Allaah 7

21- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad na al-Husayn bin Yahyaa bin ´Ayyaash ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy ametuhadithia: ´Aliy bin ´Abdillaah bin Mubashshir ametuhadithia: Ahmad bin Sinaan al-Qattwaan ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa al-´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

“Kuna mwanamume alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) (az-Za´faraaniy amesema: “Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… “) na akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) atawabeba viumbe kwenye kidole, mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, miti kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 56-58
  • Imechapishwa: 05/11/2017