21. Bora ni kuacha kufanya al-´Azl

19- Lililo bora ni kuacha kufanya al-´Azl

Lakini hata hivyo kuacha kufanya hivo ndio bora kutokana na yafuatayo:

1- Kunamletea madhara mwanamke kwa kumkosesha kustarehe. Endapo mwanamke atamkubalia basi kuna yafuatayo:

2- Yanakosekana baadhi ya malengo ya ndoa. Nayo ni kukithirisha kizazi cha Ummah wa Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Oeni wanawake wenye kuzaa sana na wenye mahaba, kwani hakika mimi nitajifakhari kwa ajili yenu siku ya Qiyaamah.”[1]

Kwa ajili hiyo ndio maana wakati alipoulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu al-´Azl, alifananisha hilo na “uuaji wa siri wa watoto wachanga” na akasema:

“Hilo ni uuaji wa siri wa watoto wachanga.”[2]

[1] Ahmad na at-Twabaraaniy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri Swahiyh. Vilevile kaipokea Ibn Hibbaan kutoka kwa Anas na ina shawahidi zengine ambazo tutazitaja katika masuala ya 19.

[2] Ameipokea Muslim (04/161), at-Twahaawiy katika “al-Mushkil” (02/370-371), Ahmad (06/361) na (434), al-Bayhaqiy (07/231) kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub aliyesema: Amenihadithia Abul-Aswad, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa ´Aaishah, kutoka kwa Jadhaamah bint Wahb…

Kuna baadhi ya watu wamefikiri kuwa inapingana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd iliyotangulia katika ukurasa wa 52 kwa tamko:

“Mayahudi wamedai kuwa al-´Azl ni aina ndogo ya kuua.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wamesema uongo mayahudi. Wamesema uongo mayahudi. Iwapo Allaah angelitaka kumuumba basi usingeliweza kumzuia.”

Hakuna kupingana kati ya hizo mbili kama walivyobainisha wanachuoni wahakiki. Bora ya yaliyosemwa katika kuzioanisha ni maneno ya Haafidhw Ibn Hajar (09/254):

“Kuoanisha kati ya uongo wa mayahudi pale waliposema:

“al-´Azl ni aina ndogo ya kuua.”

na kati ya kuthibitisha ya kwamba jambo hilo ni aina ya uuaji wa siri katika hadiyth ya Jadhaamah pale kuliposemwa:

“Hilo ni uuaji wa siri wa watoto wachanga.”

linapelekea ni uuaji lakini hata hivyo ni mdogo ukilinganisha na kumzika mtoto baada ya kuzaliwa kwake na akawa hai. Hivyo hilo halipingani na maneno yake:

“al-´Azl ni aina ndogo ya kuua.”

Hakika hilo linafahamisha ya kwamba kimsingi haliko katika hukumu ya uwazi. Hili halipelekei katika hukumu zozote. Amelifanya kuwa ni uuaji mdogo kwa njia ya kule kushirikiana kwa mawili hayo kumzuia mtoto. Kuna baadhi yao wamesema ya kwamba maneno yake:

“Ni uaaji wa siri.”

yamepokelewa kwa njia ya kufananisha. Kwa sababu ni kuzuia njia ya uzazi kabla ya kufika kwake. Ndipo akafananisha na kuuawa kwa mtoto baada ya kufika kwake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 134-136
  • Imechapishwa: 18/03/2018