3- Kufa usiku wa kuamkia siku ya ijumaa au mchana wake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna muislamu yeyote anayekufa siku ya ijumaa au usiku wa kuamkia ijumaa isipokuwa Allaah atamsalimisha na fitina ya kaburi.”

Ameipokea Ahmad (6582-6646) kupitia njia mbili kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar na at-Tirmidhiy kutoka katika moja ya njia mbili. Hadiyth hiyo ina ushahidi kupitia kwa Anas, Jaabir bin ´Abdillaah na wengineo. Kwa hivyo Hadiyth kwa njia zake zote ima ni nzuri au Swahiyh[1].

[1] Rejea katika ”Tahfat-ul-Ahwadhiy” na ”al-Mishkaah” (1367).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 30/01/2020