al-´Ayyaashiy amesema wakati alipofasiri Kauli ya Allaah (Ta´ala):

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

“Tuongoze njia iliyonyooka.”[1]

“Daawuud bin Farqad amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah [Ja´far as-Swaadiq] ambaye amesema: “Maana yake ni kiongozi wa waumini.”

Amesema katika Kauli ya Allaah (Ta´ala):

غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ

“… si [ya wale] walioghadhibikiwa wala waliopotea.”[2]

“Mu´aawiyah bin Wahb ameeleza kuwa alimuuliza Abu ´Abdillaah kuhusu Aayah hiyo. Akasema: “Ni mayahudi na manaswara”. Kuna mtu mwingine amepokea kutoka kwa Ibn Abiy ´Umayrah ambaye ameeleza ya kwamba amesema: “Namna hii ndivyo ilivyoteremshwa. Walioghadhibikiwa ni fulani, fulani, fulani, maadui na wapotofu wenye shaka wasiowatambua maimamu.”[3]

Anakusudia kuwa Abu ´Abdillaah Ja´faar as-Swaadiyq ndio kasema hivo. Allaah Amemtakasa kucheza na Qur-aan kwa njia kama hiyo ya kiyahudi. Je, unajua ni nani huyu Raafidhwiy Baatwiniy anayemkusudia wakati anaposema fulani, fulani na fulani? Anamkusudia Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan ambao ndio viumbe bora baada ya Mitume. Nafasi yao inajulikana katika Uislamu.

Maadui dhahiri ni kuwa maadui wa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa mujibu wa Raafidhwah, ni Maswahabah na wale wenye kuwafuata.

al-Faatihah iliteremshwa Makkah. Ni kwa nini Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan walihajiri na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa kama wameghadhibikiwa? Ni kwa nini alimchukua Abu Bakr kwenda naye pangoni wakati wa Hijrah? Ni kwa nini alioa msichana wa Abu Bakr na ´Umar? Ni kwa nini aliwaozesha wasichana wake wawili kwa ´Uthtmaan? Ni kwa nini alikuwa akiwachukua pindi anaposafiri, anapokuwa nyumbani na kupigana vita? Ni kwa nini alikuwa akimtanguliza Abu Bakr aongeze Swalah? Kwa nini alimwacha aongoze mahujaji katika mwaka wa 9 na ni kwa nini alimwacha akawaongoza Maswahabah wakati alipokuwa mgonjwa?

Ni kwa nini alitaamiliana na Maswahabah wa Allah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) namna hii ikiwa anajua ya kwamba wameghadhibikiwa na wamepotea? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba huku ni kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye asingeliweza hata kukubali yaliyo chini ya haya kwa mara mia!

[1] 01:06

[2] 01:07

[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/24).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 19/03/2017