7- Hukumu ya watoto wanaozaliwa na mwanamke wa Kiislamu aliyeolewa na mtu asiyeswali:

Kuhusiana na mama, ni watoto wake kwa hali yoyote ile. Kuhusu baba, ni watoto wake vilevile kwa mujibu wa maoni yasiyoonelea kuwa asiyeswali ni kafiri. Kwa mujibu wao wanaonelea kuwa ndoa yao ni sahihi. Kuhusiana na maoni sahihi yanayosema kuwa ni kafiri hali inaweza kupambanuliwa ifuatavyo:

1- Ikiwa mume hajui au anaonelea kuwa ndoa yake ni sahihi, watoto wanazingatiwa kuwa ni wa kwake. Kwa mujibu wake anaonelea kuwa jimaa ni halali na kwa hiyo jimaa hiyo inazingatiwa kuwa ni yenye utata. Watoto wanaotokamana na jimaa yenye utata wananasibishwa kwa baba.

2- Ikiwa mume anatambua na kuonelea kuwa ndoa yake ni batili, watoto hawazingatiwi kuwa ni wa kwake. Katika hali hii watoto watakuwa wameumbwa kutokamana na maji ya ambaye anaonelea kuwa jimaa yake ni haramu kwa sababu amefanya nayo na mwanamke ambaye si halali kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 22/10/2016