20. Warithi wa Khawaarij hii leo


Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Katika mlango wa matishio ya Allaah wako kati ya Murji-ah na Wa´iydiyyah.”

Tumeshatangulia kuwaelezea Murji-ah. Ni wale wanaosema kuwa matendo hayaingii ndani ya uhakika wa imani. Wa´iydiyyah ni wale wanaotendea kazi maandiko ya matishio na wanamhukumu ukafiri mwenye kutenda dhambi kubwa na kumtoa nje ya Uislamu. Haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Wana warithi hii leo miongoni mwa wale wenye kujifanya ni wanachuoni na wajinga ambao hawajui kuzitumia dalili, hawazielewi dalili na wala hawairejei ´Aqiydah ya Salaf. Matokeo yake wanayachukua maandiko na kucheza nayo na wanawahukumu watu ukafiri na kutoka nje ya dini. Baada ya hapo matokeo yake wanabeba silaha dhidi yao kama alivofanya babu yao katika Huruuriyyah. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 39
  • Imechapishwa: 10/03/2021