20. ´Ubaydah bin al-Haarith anatumwa kwenda Thaniyyat-ul-Marah

Rabiy´ ath-Thaniy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtuma ´Ubaydah bin al-Haarith bin al-Muttwalib akiwa pamoja naye wapandaji sitini au thamanini wa Muhaajiruun kwenda katika maji kusini mwa Hijaaz kuhusu Thaniyyat-ul-Marah. Huko wakakutana na kundi kubwa la Quraysh wakiwa na ´Ikrimah bin Abiy Jahl kama kiongozi wao. Imesemekana vilevile kwamba walikuwa na Mikraz bin Hafsw kama kiongozi wao. Hakukutokea kati yao vita isipokuwa tu wakati huo Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) aliwarushia washirikina mshale. Yeye ndiye alikuwa wa kwanza kurusha mshale katika njia ya Allaah. Siku hiyo ndipo al-Miqdaad bin ´Amr al-Kindiy na ´Utbah bin Ghazwaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa) walikimbia kutoka kwa washirikina na kwenda kwa waislamu.

Misafara hii miwili ya kijeshi ndio ikawa ya kwanza ambayo ilitumwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo kuna maoni tofauti kuhusu ni msafara upi ulioanza kutumwa. Kuna maoni yanayosema kwamba yote miwili ilikuwa mwaka wa kwanza baada ya kuhajiri. Haya ndio maoni ya Ibn Jariyr at-Twabariy na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 25/04/2018