20. Ni wajibu kulipa deni la Ramadhaan kabla ya kuingia Ramadhaan nyingine


Swali 20: Baadhi ya wanawake wanaingiliwa na Ramadhaan ya pili ilihali hawajafunga Ramadhaan iliotangulia. Ni kinachowawajibikia?

Jibu: Ni lazima kwao kutubu kwa Allaah kutokana na kitendo hichi. Haijuzu kwa ambaye analo deni la Ramadhaan kuchelewesha mpaka katika Ramadhaan ya pili pasi na udhuru. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Nilikuwa nadaiwa funga na nashindwa kuilipa mpaka katika Sha´baan.”

Hii inafahamisha kwamba haifai kuchelewesha mpaka baada ya Ramadhaan ya pili. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa aliyofanya na pia alipe masiku aliyoyaacha baada ya Ramadhaan ya pili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 04/07/2021