20. Ni ipi hukumu hedhi ikijitokeza katikati ya mchana wa Ramadhaan?


Swali 20: Ni ipi hukumu hedhi ikijitokeza katikati ya mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Ni lazima kwake kujizuia kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni kwa sababu ameondokewa na udhuru wa Kishari´ah. Hata hivyo ni lazima kwake kuilipa siku hiyo kama ambavo lau mwezi mwandamo utathibiti mchana wa Ramadhaan. Basi katika hali hiyo waislamu watatakiwa kujizuia siku iliyobaki na wailipe siku hiyo kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Kadhalika msafiri atapofika katika mji wake katikati ya mchana wa Ramadhaan basi ni lazima kwake kujizuia kutokana na maoni yenye nguvu zaidi ya wanachuoni kwa sababu ameondokewa na hukumu ya safari. Hata hivyo atatakiwa kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 03/05/2019