20. Ngazi nne za mawalii wa Allaah


Salaf na maimamu wa Ummah na mawalii wengine wa Allaah wameafikiana juu ya kwamba Mitume ni wabora kuliko mawalii ambao sio Mitume. Allaah amewapangia waja Wake wenye furaha walioneemeshwa ´ngazi nne`. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli na mashahidi na waja wema – na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao.”[1]

Wanazo karama ambazo Allaah huwakirimu kwazo waja Wake wenye kumcha. Mawalii wa Allaah wabora karama zao inakuwa kwa lengo la kusimamisha hoja katika dini au kwa sababu waislamu wanahitajia jambo hilo, hali kadhalika ndivo ilivyokuwa miujiza ya ya Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Karama za mawalii wa Allaah zimepatikana kutokana na baraka za kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Ukweli wa mambo ni kwamba ni moja katika miujiza ya Mtume…

Aidha itambulike kuwa karama zinakuwa kwa kiasi cha haja ya mtu. Ikiwa anazihitajia kutokana na udhaifu wa imani yake, anahitajia kwa ajili ya kumtia nguvu imani yake na kumtekelezea haja yake na yule ambaye ana uwalii kamilifu zaidi ni mwenye kujitosheleza kutokamana na hayo. Hivyo mfano wa hayo hayaji kwa ajili ya kuonyesha ngazi yake ilihali amejitosheleza nayo na sio kwa sababu ya upungufu wa uwalii wake. Kwa ajili hiyo mambo haya kwa Taabi´uun yalikuwa mengi kuliko kwa Maswahabah. Hilo ni tofauti na yule anayepitisha mambo haya yasiyokuwa ya kawaida kwa ajili ya kuwaongoza viumbe na kuhitajia kwao. Watu hawa wana ngazi za juu zaidi…

[1] 04:69

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 24/06/2021