Vilevile wanaanini kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui mambo yaliyofichikana isipokuwa yale aliyofunuliwa na Allaah. Hamiliki juu ya nafsi yake wala nafsi ya mwengine madhara wala manufaa. Allaah (Ta´ala) amemwamrisha afikishe ujumbe huo kwa Ummah:

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ

“Sema: “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah na wala kwamba najua mambo yaliyofichikana na wala sikuambieni kwamba mimi ni Malaika.”[1]

Kazi yake ni ipi?

إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ

“Sifuati isipokuwa yale nilofunuliwa Wahy.”[2]

Mwenye kudai kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anajua kitu katika mambo ya ghaibu – mbali na yale aliyofunuliwa na Allaah – basi ni kafiri aliyemkufuru Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu amemkadhibisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrishwa aseme maneno yatayosomwa hadi siku ya Qiyaamah:´

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ

“Sema: “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah na wala kwamba najua mambo yaliyofichikana na wala sikuambieni kwamba mimi ni Malaika.”[3]

[1] 06:50

[2] 06:50

[3] 06:50

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 32
  • Imechapishwa: 19/08/2019