20. Msamaha wa Allaah na ukarimu wake


Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ

Mmehalalishiwa usiku wa kufunga swawm kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah anajua kwamba mlikuwa mkizihini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni tawbah yenu na akakusameheni.”[1]

Mwanzoni mwa Uislamu ilikuwa inajuzu kwa mfungaji aliyekata swawm kula, kunywa na kufanya jimaa midhali hajaswali ´Ishaa wala hajalala. Akilala au akaswali ´Ishaa basi inaharamika kwake kufanya jimaa, kula na kunywa. Halafu Allaah akataka kuonyesha huruma Yake juu ya waislamu.

Kuna mwanamume kutoka katika Answaar alikuwa akifanya kazi shambani kwake mpaka ´Ishaa. Katika wakati huo walikuwa wakibeba maji juu ya ngamia na wakiimwagilia maji mitende. Walikuwa wakifanya kazi mashambani kwa ajili ya kujipatia riziki. Alipofika nyumbani magharibi akaomba chakula. Mke wake akaenda kumtengenezea chakula. Aliporudi akamkuta amelala ambapo akamwambia kuwa chakula kimekuwa ni haramu kwake. Akaendelea na swawm yake na akaamka hali ya kuwa hana kitu tumboni. Asubuhi akaenda shambani kwake kufanya kazi na akaanguka na kupoteza fahamu wakati wa Dhuhr ambapo akabebwa kupelekwa nyumbani.

Mfano wa hayo yamemtokea ´Umar bin al-Khattwaab na waumini wengine (Radhiya Allaahu ´anhum) waliokuwa wamewaingilia wake zao. Siku moja ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alichelewa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akarudi nyumbani ambapo akataka kufanya jimaa na mke wake. Mke wake akamweleza kuwa amelala. Akafikiri kuwa anajipa udhuru na kuzua ambapo akamwingilia kwa kutokupenda kwake. Pindi alipomhakikishia ya kuwa kweli alilala akasikitika. Asubuhi akamwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutarajia atapata makimbilio kutoka kwa Allaah kisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akateremsha:

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ

“Mmehalalishiwa usiku wa kufunga swawm kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao.”[2]

Kuwakaribia wake kunamaanishwa jimaa na ile michezo ya kabla yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swawm ni kinga. Pindi mmoja wenu atapokuwa amefunga asizungumze upuuzi upuuzi (فلي يرفث) wala asigombane. Mtu akimtukana aseme: “Mimi nimefunga.”

Katika maneno Yake (Ta´ala):

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ

“Mmehalalishiwa usiku wa kufunga swawm kuwaingilia wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao.”[3]

 hapa kuna miujiza ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa waja Wake wadhaifu na waumini.

Allaah (Ta´ala) amesema:

عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ

“Allaah anajua kwamba mlikuwa mkizihini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni tawbah yenu na akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni aliyokuandikieni Allaah.”[4]

 Bi maana jimaa, kula na kunywa.

Hapana shaka kwamba hapa kuna fadhila kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) juu ya waja Wake waumini kwa kule kuwasamehe madhambi yao yaliyotangulia. Kisha akawaacha wale, kunywa na kufanya jimaa katika nyusiku za funga mpaka kuingia kwa alfajiri.

[1] 02:187

[2] 02:187

[3] 02:187

[4] 02:187

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 34-37
  • Imechapishwa: 02/06/2017